Jiografia:
Wilaya ya Tabora inapatikana katika vipimo vya latitude 4°52' na 5°9' Kusini na Longitude 32° 29' na 33° 00' Mashariki. Eneo kubwa la Wilaya lipo kati ya mwinuko wa meta 1,000 na 1,500 juu ya usawa wa bahari. Wilaya ya Tabora imezungukwa na Wilaya za Uyui upande wa Magharibi, Kaskazini na Mashariki. Upande wa Kusini Tabora inapakana na Wilaya ya Sikonge. Wilaya inayo Halmashauri moja ambayo ni Manispaa ya Tabora, na hiyo ndiyo Makao Makuu ya Mkoa wa Tabora.
Utawala:
Wilaya inazo tarafa 2, Kata 25 ambapo 13 kati ya hizo zipo mjini na 12 zipo nje ya mji; vijiji 30, Vitongoji 116 na Mitaa 118. Wilaya inayo Halmashauri moja tu yenye hadhi ya Manispaa.
Jedwali : Mgawanyo wa maeneo ya Utawala
Wilaya
|
Majimbo ya Uchaguzi |
Tarafa |
Kata |
Vijiji |
Mitaa |
Vitongoji |
Tabora |
1 |
2 |
25 |
30 |
118 |
116 |
Ili kuimarisha utawala bora ujenzi wa ofisi za kata unapewa kipaumbele katika manispaa ya TABORA. Picha hapo juu inaonesha ujenzi wa Ofisi ya kata ya Cheyo. Pia Majengo mengine yanajengwa katika kata za Ifucha, Ikomwa na Mbugani.
Idadi ya Watu:
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Manispaa ya Tabora ina jumla ya wakazi 226,999. Wanaume ni 111,361 na wanawake ni 115,638. Idadi hii ni kutokana na ongezeko kwa kiwango cha asilimia 2.36 kwa mwaka. Wastani wa watu katika kaya ni 4.7. Idadi ya watu, kaya na msongamano wao katika Wilaya ni kama inavyoonesha katika jedwali lifuatalo:-
Jedwali : Hali ya Mtawanyiko wa Idadi ya Watu Wilaya ya Tabora
ENEO KTK KM2 |
KASI YA ONGEZEKO LA WATU KWA MWAKA % |
UKUBWA WA KAYA
|
IDADI YA WATU |
IDADI YA KAYA |
|||
2012 (Sensa) |
Kwa Km. ya Mraba |
2012 (Sensa) |
2013
|
||||
2012 |
2013 |
||||||
1,092 |
2.3 |
4.7 |
226,999 |
172 |
208 |
39,368 |
69,560 |
Hali ya Uchumi na Maendeleo ya Wilaya:
Uchumi wa Wilaya ya Tabora kwa sehemu kubwa unategemea kilimo, mifugo na Biashara. Kilimo na mifugo huchangia asilimia 49 ya uchumi wa Wilaya na Biashara asilimia 28.5. Aidha, viwanda vidogo vidogo huchangia asilimia 13.01 na shughuli za ofisini asilimia 8.6.
Pato la Wilaya limepanda kutoka Tsh. 383,250/= Mwaka 2007 hadi Tshs.470,983 Mwaka 2012. Ambalo lipo chini ya pato la Taifa la 558,400. Hii ni sawa na ongezeko la Tshs. 87,783 sawa na asilimia 23.
Wilaya inaendelea na jitihada za kukuza uchumi kwa kutekeleza mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA) pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 kwa kushirikisha wananchi na Wadau mbalimbali ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2025, Malengo ya Milenia, na MKUKUTA.
SEKTA YA AFYA
Huduma za Afya (Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati)
-
Hospitali moja (1) inamilikiwa na Serikali ya Mkoa.
-
Vituo vya Afya 3 vinamilikiwa na Mashirika ya Dini, vinavyofanya kazi ni viwili na kimoja kimefungwa kwa kutokidhi vigezo.
-
Zahanati 17 zinazomilikiwa na Halmashauri
-
Zahanati 10 za Taasisi za Serikali (zinafanya kazi)
-
Zahanati 4 za binafsi (1 imefungwa na wizara)
-
Zahanati 3 za Taasisi za dini (1 imefungwa na wizara)
Hakuna Hospitali ya wilaya wala Kituo cha Afya kinachomilikiwa na Halmashauri. Hata hivyo Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ni miongoni mwa vipaumbele vya Wilaya ya Tabora.
Ujenzi wa nyumba ya mtumishi (2:1) zahanati ya Umanda
Mwaka 2013/2014 mpango mkakati wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya umeanza ambapo serikali kuu imetoa jumla Tash 150,000,000.00, Uongozi wa Wilaya umefanya vikoa kuhusisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhamasisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, hatua iliyofikiwa ni upatikanaji wa kiwanja eneo la Ipuli.
Idadi ya Hospitali, vituo vya afya na zahanati
Wilaya
|
Vituo vya kutolea hudumam Manispaa ya Tabora
|
|||||
|
2012 |
2013/2014 |
||||
Manispaa ya Tabora
|
Hospitali
|
Vituo vya afya
|
Zahanati
|
Hospitali
|
Vituo vya afya
|
Zahanati
|
1
|
2
|
35
|
1
|
2
|
32
|
NB: Hospitali hii (1) ya Kitete ni ya Mkoa wa Tabora.
Mradi wa ujenzi wa OPD kituo cha afya Itetemia. Kituo hiki kimekamilka na kinafanya kazi
Watumishi idara ya Afya:
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ina upungufu mkubwa wa rasilimali watu katika vitengo vyake vyote. Watumishi katika kitengo cha kinga ikama ni 68, waliopo ni 54 na upungufu ni watumishi 14. Kitengo cha Tiba ikama ni 337 waliopo 225 upungufu ni 112, hivyo kufanya jumla ya upungufu wa watumishi kuwa 126.
Nyumba ya mtumishi (2:1) Zahanati ya Itetemia