MKOA WA TABORA WAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BIL 296.2 KWA MWAKA 2018/2019
MKOA wa Tabora umepitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti ya bilioni 296.2 kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mapendekezo hayo yamepitishwa jana na Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tabora.
Akiwasilisha mapendekezo ya bajeti hiyo Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Mipango) Hajjat Rukia Manduta alisema kati ya fedha hizo bajeti ya Sekretarieti ya Mkoa(RS) ni bilioni 11.6 na Mamlaka ya Serikali za Mitaa(MSM) ni bilioni 284.6.
Alisema kati ya fedha hizo 203.3 ni mishahara, matumizi mengineyo ni bilioni 23.3 na miradi ya maendeleo bilioni 69.6 .
Hajjat Rukia alisema mwaka ujao wa fedha mapato ya ndani yatakuwa bilioni 35.8 na mishahara itakuwa bilioni 33.7.
Alisema kwa MSM bilioni 195.2 ni mishahara, matumizi mengineyo bilioni 21.6 , miradi ya maendeleo ni 67.7 ambapo fedha za ndani ni shilingi bilioni 34.4 na fedha za nje ni 33.2.
Kwa upande wa RS alisema kuwa mishahara ni bilioni 8, matumizi mengineyo ni bilioni 1.7, miradi ya maendeleo ni bilioni 1.8 na fedha za ndani ni bilioni 1.3 na fedha za nje ni milioni 536.3.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa