0. UTANGULIZI
Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Misitu ya Miombo (SFM) unatekelezwa kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2013 hadi 2018.Ufadhili wa Mradi huu ni kutoka Mfuko wa Mazingira Duniani kwa kukasimu usimamizi wa fedha katika Shirika la Maendeleo la Dunia (UNDP) ofisi ya Tanzania iliyopo Dar es Salaam. Kwa upande mwingine Mradi umefadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa kukasimu majukumu katika ofisi ya Makamu wa Rais ambapo utekelezaji wa shughuli unasimamiwa na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora akishirikiana na Katibu Tawala Mkoa wa Katavi.Utekelezaji wa shughuli katika ngazi ya jamii unafanywa na Halmashauri za Wilaya ya Kaliua,Urambo na Uyui kwa Mkoa wa Tabora na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwa Mkoa wa Katavi. Aidha Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Tathmini ya Rasilimali za Maliasili (IRA) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii Idara ya Misitu na Nyuki ilipewa jukumu la uangalizi na ushauri wa kitaalam katika utekelezaji.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa