Mkuu wa wilaya ya Uyui Mh. Zakaria Mwansasu amemkabidhi mti mwananchi wa kijiji cha Nzubuka wilayani Uyui kama moja ya jidihada za kumuunga mkono Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mh.Dkt. Batilda Salha Burian katika kuhakikisha zoezi La upandaji miti linatekelezeka kwa usahihi.Akikabidhi mti huo, DC Mwansasu amewataka wanakijiji wa Nzubuka kutunza mazingira na vyanzo vya maji kwa kupanda miti. Tayari serikali kwa kushirikiana na wadau wa mazingira watahakikisha elimu ya mazingira inatolewa kwa wananchi.
Kwa Mwaka huu Mkoa wa Tabora unatarajia kupanda miti milioni 12, na Kauli mbinu ya mkoa wa Tabora inasema “Maji ni Uhai na Mti ni Maisha”
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa