• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
      • Community development
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

DKT. MBOYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA WAKUU WA IDARA ZA RASILIMALI WATU TABORA: ASISITIZA KUJENGA MAHUSIANO YENYE AFYA NA MOTISHA MAHALA PA KAZI.

Posted on: February 6th, 2026



Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya, amefungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka halmashauri zote za mkoa wa Tabora, chenye lengo la kuboresha ufanisi wa utendaji katika utumishi wa umma. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa.


Akitoa neno la utangulizi, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Upendo Joseph Haule, alisema kuwa madhumuni makuu ya kikao hicho ni kuimarisha utendaji kazi, kuongeza tija na kuhakikisha huduma bora zaidi zinatolewa kwa watumishi na wananchi wa mkoa wa Tabora.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Dkt. Mboya aliwapongeza wakuu wa idara hao kwa mchango wao mkubwa katika kusimamia rasilimali watu, na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kujituma. Aliwataka watalaam hao kuhakikisha wanahudumia wananchi kwa weledi na nidhamu, ili kuendana na matarajio ya Serikali.


Dkt. Mboya alieleza kuwa Serikali inalenga kujenga utumishi wa umma uliotukuka na wenye maadili, unaozingatia sheria, taratibu na kanuni za kazi. “Tunahitaji kuona utumishi wa umma uliotukuka. Tunataka kuwa na watumishi wa umma ambao ni kioo cha jamii. Nendeni mkajenge mahusiano yenye afya na motisha mahala pa kazi,” alisisitiza.


Kwa upande wake, Bi. Haule alieleza kuwa kikao hicho kitajadili ajenda 12 muhimu zinazohusu masuala ya usimamizi wa rasilimali watu. Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni pamoja na usimamizi wa mfumo wa E-Utendaji, ufuatiliaji wa masuala ya kinidhamu kwa kuzingatia sheria, usafishaji wa taarifa za watumishi katika mifumo ya kielektroniki, mapitio ya mwongozo wa kujitolea kazini, pamoja na taratibu za uhamisho wa watumishi.


Aliongeza kuwa majadiliano hayo yanalenga kuleta maboresho ya kiutendaji, kuongeza uwajibikaji na kuhakikisha kuwa utumishi wa umma unakuwa na tija zaidi kwa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.


Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABORA KWENDA KUNUFAIKA NA ZOEZI LA UPIMAJI NA UTAFITI WA AFYA YA UDONGO.

    February 06, 2026
  • VIONGOZI TABORA WAHANI MSIBA WA MFANYABIASHARA MZALENDO MZEE NASSORO HAMDAN SEIF.

    February 06, 2026
  • DKT. MBOYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA WAKUU WA IDARA ZA RASILIMALI WATU TABORA: ASISITIZA KUJENGA MAHUSIANO YENYE AFYA NA MOTISHA MAHALA PA KAZI.

    February 06, 2026
  • TABORA: WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WAKARIBISHA MWAKA 2026, NA KUWAAAGA WASTAAFU

    January 31, 2026
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice
  • Migration Tanzania

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa