Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Urambo Bi Grace Quintine amezindua kampeni ya kufundisha maadili katika shule ya Msingi na sekondari kwa lengo la kutokomeza Mimba mashuleni. Ameeleza kuwa, bado wilaya ya Urambo inakabiliwa na changamoto ya mmomonyoko wa maadili jambo ambalo linapelekea watoto wengi wa kike waliopo mashuleni hujiingiza kwenye vitendo vinavyopelekea kuongezeka kwa mimba mashuleni humo.
Aidha. Bi. Grace ameongeza kuwa, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi watahakikisha suala la utolewaji wa elimu kwa Umma linapewa Kipaumbele na kutoa wito kwa wazazi na walezi kutumia muda wao kukaa na watoto wao na kutoa elimu ya maadili kwa watoto hao.
Kampeni hii imejikita katika kuwaeleza watoto uhalisia wa maisha ili waepukane na vikwazo ambavyo vinaweza kuwapekea watoto wa kike kujiingiza kwenye vitendo vinavyokiuka maadili.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa