Katika kikao hiko Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa Vyombo vinavyohusika na usafirishaji kuzingatia suala la utozwaji wa nauli zilizopangwa na utoaji wa tiketi ili kuepukana na usufumbusu. Alisema kuwa “Serikali iliongeza viwango vya nauli kwa mabasi yote yanayotoa huduma ya usafiri nchini kutokana na ongezeko la gharama za uendeshaji, viwango hivyo vipya vilianza kutumika kuanzia tarehe 08/12/2023. Viwango vya nauli vimepangwa kwa kuzingatia hali ya barabara na madaraja ya mabasi”
Na kuongeza kuwa, Magari yanayotoa huduma ya usafiri ndani ya mkoa yanapaswa kutumia tiketi za kuandikwa kwa mkono sambamba na utozwaji wa nauli zilizopangwa na Serikali.
Aidha, Mhe. Batilda Salha Burian ameziagiza mamlaka husika kudhibiti wimbi la wapiga debe Katika stendi za mabasi ambao wamekuwa kero kwa baadhi ya wasafiri ikiwemo kuongezeka kwa vitendo vya uharifu na utozwaji wa nauli zisizopangwa. Amesema kuwa “hivi sasa stendi zetu zina wapigadebe wapatao 1,200. Uwepo huu wa idadi kubwa ya wapigadebe linachangia ongezeko la vitendo vya kihalifu, ikiwemo wizi na utapeli, ulanguzi wa nauli na uuzaji wa tiketi kwa mabasi yasikuwepo kabisa”
Na aliongeza kusisitiza kwamba Halmashauri kwa kushirikiana na Vyombo vya ulinzi itumie sheria zake kudhibiti wimbi hilo kwa kutoa vitambulisho.
Afisa mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) Ndugu. Nelson Mmari amekiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto kwenye sekta usafirishaji likiwemo suala la upandishwaji wa nauli kiholela licha ya kuwepo kwa nauli zilizopangwa.
Naye, Kamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Tabora (RTO) SP Peter Magayane amemuahaidi Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuyafanyia kazi maagizo yote aliyopewa na kuongeza kuwa, asilimia Kubwa ya changamoto zilizopo kwenye sekta hii inachangiwa na wapiga debe wachache wanaokiua Sheria na taratibu zilizowekwa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa