Akihutubia wananchi waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa ameweka bayana kuwa, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na wafanya biashara wote kwa kuunda sera bora zenye kuleta maslahi kwa wafanya biashara wote.
“Napenda niwaahidi kuwa, Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Dkt Samia S. Hassan, siku zote itakuwa bega kwa bega nanyi na itawashirikisha kama ambavyo mmejionea kwa nyakati tofauti tunahuisha Sera na Sheria za kodi ili kuondoa au kupunguza changamoto mnazokumbana nazo”. Alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Sambamba na hilo, Mhe. Dkt Batilda Burian, ameleza kuwa, Serikali inatambua mchango wa walipa kodi katika taifa letu na mkoa kwa ujumla, na kwamba msingi mkuu wa maendeleo kwa taifa lolote ni kodi zinazokusanywa.
“Nchi nyingi duniani zinategemea kodi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake. Nchi yetu ni moja wapo kati ya nchi hizo zinazotegemea kodi kwa ajili ya kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo” aliongeza Dkt. Batilda
Aidha Dkt. Batilda ameokana kukerwa na tabia ya baadhi ya wafanya biashara kutokutumia mashine za EFD ambazo hutumika kutolea risiti pale mauzo yanapofanyika, na bado kunwa wafanya Biashara pia hutoa risiti feki na wakati mwingine hutoa risiti inayotofautiana na mauzo halisi.
“kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wafanya biashara wachache wasio waaminifu hasa katika suala zima la kutoa risiti sahihi za EFD. Tabia iliyopo sasa hivi ni ama kutoa risiti pungufu ya fedha aliyolipia mnunuzi au kutokutoa kabisa risiti. Baadhi hutumia risiti moja kusindikiza mizigo kutwa kwenda kwa wateja na wengine hutoa risiti kutoka kwenye mashine bandia ambazo haziko kwenye mfumo wa TRA.” Alisema Dkt. Batilda.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akihutubia wananchi wa Tabora kwenye Hafla ya kukabidhi tuzi kwa Walipa kodi bora wa mwaka kutoka Mkoa wa Tabora iliyofanyika katika Ukumbi wa Nazaleth, Manispaa ya Tabora Mkoani Tabora Disemba 6, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akikamilisha zoezi la utoaji wa tunzo kwa walipa kodi bora wa mwaka kutoka Mkoa wa Tabora kwenye Hafla ya kukabidhi tuzo kwa Walipa kodi bora wa mwaka kutoka Mkoa wa Tabora iliyofanyika katika Ukumbi wa Nazaleth, Manispaa ya Tabora Mkoani Tabora Disemba 6, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa