Picha zikionesha Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndugu Abdalla Shaib akitembelea Kikundi cha Vijana cha Twende Pamoja kilichopo Usoke Wilayani Urambo. Ambapo kikundi hiko kilipatiwa jumla ya shilingi milioni 18.9 kama sehemu ya mkopo wa asilimia 4 ya mapato ya ndani ya Halmashauri na kufanikiwa kuanzisha mradi wa Usafirishaji wa abiria kwa pikipiki (Bodaboda)
Mradi huu wa vijana ni miongoni mwa miradi nane (8) ambayo imepitiwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo. Ambapo Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Kenani Kihongosi aliupokea kutoka Wilaya ya Kaliua
Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Tabora Septemba 14, 2023 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge. ambapo utahitimisha mbio zake ukiwa umezindua jumla ya miradi 50 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2 na kukabidhiwa Mkoa wa Singida Septemba, 21, 2023.
Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa