WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasi na Utalii wameitaka Serikali ipeleke fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora.
Mradi huo ambao umekwama kumalizika kwa miaka saba unahitaji kiasi cha shilingi bilioni 1.1 ili kukamilika.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Massay alisema mradi umesimama siku nyingi ni vema Serikali ikatoa fedha za kumalizia ulipokwamia ili wanachuo waanze kunufaika.
Alisema fedha nyingi imeshatolewa na jengo bado halijakamilika jambo ambazo lizidi kusababishia wanachuo kukosa sehemu ya kujisomea.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauye alisema ni vema Serikali ikatenga fedha katika bajeti ijayo ili ikiwezekana wakamilishe ujenze na ianze kutumika.
Alisema kila mwaka Bunge linapitisha fedha lakini hakuna kinachoendelea kwenye ujenzi wa mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la Longido Dkt. Steven Kiruswa alikishauri Chuo kuangalia uwezekano wa kuandika andiko mradi kwa ajili ya kupata fedha zitakazowawezesha kukamilisha ujenzi huo.
Mbunge Jimbo la Chambani Yussuf Salim Hussein alihoji uwezo wa Mkandarasi wa Jengo hili alipiga ripu kabla ya kueezeka ambapo fedha hizo angetumia kuezeka.
Alisema ni vema Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wanapopewa kazi ya kusimamia wakafanya vizuri badala kufanya kwa kiwango ambacho hakiridhishi .
Naye Mbunge wa Jimbo la Kaliua Magdalena Sakaya alisema ni vema Wizara ikaona umuhimu wa kukamlisha jengo hilo kwa ajili ya kuzalisha watalaamu ili kuziba mapengo kwenye Halmashauri mbalimbali hapa nchini.
Alisema wataalamu hao wanahitaji kwa ajili ya kusaidia kutatua matatizo na migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali.
Akijibu hoja za Wabunge hao Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula alisema kumekuwepo na miradi mingi ambayo inahitaji fedha ndio maana kumekuwepo uchelewaji baadhi yake kwa sababu ya ufinyu wa fedha.
Alisema miradi mingine iliyokwama inazaidi ya miaka 10 na yote inahitaji fedha ili iweze kukamilika na kuongeza kuwa Serikali ipo katika jitihada za kuikamilisha kwa kutegemea upatikanaji wa fedha.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa