• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

AMCOS TABORA ZAMPONGEZA DKT. SAMIA

Posted on: October 6th, 2023

Zaidi ya wanachama 420 kutoka vyama vya Msingi (AMCOS) Mkoani Tabora wamempongeza na kumshukuru Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha wakulima wa Tumbaku wanapata Mbolea ya Ruzuku ya kutosha na kwa wakati pasipo na changamoto zozote kama ilivyokuwa hapo awali. Hayo yamejiri Leo Oktoba 6, 2023 wakati wa Ufungaji wa Mafunzo ya Wenyeviti na Watendaji wa AMCOS zilizopo Wilayani Urambo na Kaliua.

 

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, amewahakikishia wakulima wa Tumbaku kuwa, Serikali inatambua mchango wao na hivyo ina kila wajibu wa kuhakikisha wakulima hao wanapata mbolea ya ruzuku kwa wakati ili kukuza uzalishaji wa zao la Tumbaku.

 

“Serikali inatambua mchango wa wakulima wa Tumbaku, na tayari Mhe. Rais ameshatenga fedha kwa ajili ya mbolea ya ruzuku ambayo ipo tayari na kuwafikia wakulima wakati wowote, na nitoe wito kwa wakulima kujisajili kwenye mfumo uliowekwa kwa kufuata vigezo na taratibu” Alisema Dkt. Batilda

 

Sambamba na hilo , Dkt. Batilda ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa AMCOS kuhakikisha wanawajibika kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa ili kuendesha na kusimamia vyama vya msingi.

 

“Viongozi na Watendaji wote wa Vyama vya Ushirika mnaelekezwa kusimamia na kuendesha vyama vya Ushirika kwa kuzingatia sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 ili kulinda maslahi ya wakulima wa Tumbaku” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa

 

Aidha, Mhe, Mkuu wa Mkoa, ameeleza juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika inapigania na kulinda maslahi ya wakulima wa Tumbaku kwa kuhakikisha wakulima wanapata malipo yao kwa wakati uliopangwa.

 

“Mpaka sasa kiasi cha fedha ambacho kimelipwa ni kiasi USD 141,168,519 na deni lililobaki mpaka sasa ni USD 3,563,832.6 ambapo tayari Serikali imeshatoa maelekezo mpaka kufikia tarehe 10 Oktoba, 2023 Kampuni zinazodaiwa ziwe zimeshalipa deni hilo.” Alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa.

 

Mbali na hayo Mkuu wa Mkoa alitoa maelekezo kama, Halmashauri kukaa na kamati za Pembejeo na kufanya mapitio ya bei za mbolea, pia ameeleza mikakati ya Serikali ya kutafuta wadau wa Bima za mazao ili kupambana na majanga ya mvua za mawe ambazo huathiri tumbaku kwa kiasi kikubwa.

 

 

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa