Katika kuimarisha uwajibikajina utendaji wa watumishi wa umma kwa kutumia teknolojia ya kisasa, Ofisi yaRais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana naOfisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, imeendesha mafunzo maalum ya mfumo wa e-Utendajikwa wasimamizi wa watumishi wa umma katika taasisi za umma mkoa wa Tabora yaliyofanyikakatika ukumbi wa mikutano wa Mtemi Isike Mwanakiyungi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Rais –Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Cecilia Meela alisema kuwamafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuimarisha utekelezaji wamajukumu kwa njia ya kidigitali.
“Lengo letu ni kukumbushana matumizi sahihi ya mfumo mzima wa e-Utendaji, hususankatika kipengele cha tathmini ya utendaji wa watumishi. Pia tutapitia hatua kwahatua vipengele vyote vya mfumo wa pepmis ili kutambua mafanikio yaliyopatikanana changamoto zinazojitokeza,” alisema Bi. Meela.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka kuelekea mwisho wa mwaka wa fedha2024/2025, hatua ambayo ni muhimu katika zoezi la upandishaji madaraja kwawatumishi wa umma kote nchini. “Tumejipanga kuhakikisha hakuna mtumishianayeachwa nyuma. Tunatoa wito kwa watumishi wote kuujua, kuuelewa na kuutumiakikamilifu mfumo huu,” alisisitiza.
Washiriki wa mafunzo hayo ni watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Halmashauri ya Wilaya ya Uyui pamoja nataasisi nyingine zote zinazotumia mfumo wa e-Utendaji katika mji wa Tabora.
Mafunzo hayo yameanza leo Juni 23, 2025 na yataendelea hadi Juni 26, 2025 katika wilayazote za Mkoa wa Tabora na taasisi zake. Kupitia mafunzo haya, Serikali inalengakuimarisha matumizi ya teknolojia katika utendaji kazi na kuongeza uwazi,uwajibikaji na ufanisi kwa watumishi wa umma nchini.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa