Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika kwa Mkoa wa Taborayamefanyika kwa shamrashamra wilayani Sikonge katika uwanja wa michezo waTasaf, yakihudhuriwa na mamia ya wananchi, viongozi na wadau wa maendeleo yamtoto.
Awali, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Bi. Monica Yesaya alieleza kuwamafanikio ya maadhimisho hayo yametokana na mchango mkubwa wa wadauwanaosimamia malezi ya watoto, huku akitoa rai kwa jamii kushiriki kikamilifukatika kulinda na kutetea haki za mtoto kila mahali.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Ndg. Nico Kayange aliwahimiza watoto kutiimaelekezo ya wazazi na walezi wao, ili wakue katika maadili mema na kuwa raiawema wa baadaye.
Akihutubia katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe.Paulo Chacha, Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Naitapwaki Tukai amesisitiza wajibuwa jamii nzima kuhakikisha mtoto anaishi katika mazingira salama, na hakunanafasi kwa aina yoyote ya ukatili dhidi yao.
Ametoa tahadhari kuhusu matumizi ya luninga kwawatoto bila uangalizi wa wazazi, akisisitiza kuwa baadhi ya maudhuiyanayorushwa si rafiki kwa malezi ya watoto na huweza kuathiri mienendo yao.
Katika hotuba yake, Mhe. Tukai pia aliwatakawatoto wajue haki zao na wajitambue, hasa wanapokuwa katika mazingira yakijamii, na kuhakikisha kuwa wanachukua tahadhari dhidi ya ukatili wa ainayoyote.
Maadhimishoya mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu isemayo “Hakiza Mtoto: Tulipotoka, Tulipo na Tunapoelekea,” ikiwa ni fursa yakutathmini hatua zilizofikiwa katika kulinda na kuendeleza haki za mtoto waAfrika, sambamba na kutafakari mwelekeo wa baadaye katika kujenga kizazi bora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa