Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameeleza kuwa, bado Mkoa unakabiliwa na changamoto za utoaji wa chakula mashuleni unaosababishwa na ufinyu wa bajeti zinazotolewa na halmashauri zetu. Ameyasema hayo leo Julai 6, 2023 alipokutana na kufungua kikao kazi cha viongozi na watendaji ngazi ya Mkoa na Wilaya.
Sambamba na hilo, Dkt. Batilda ametoa wito kwa watendaji wa elimu kuhakikisha wanafanya maboresho makubwa kwenye sekta ya elimu hususani suala la utoaji wa chakula mashuleni. “Ni jukumu lete la Serikali kuhakikisha suala la utoaji wa chakula mashuleni linazingatiwa ili kuendana na kasi ya Serikali katikq maboresho ya miundombinu ya elimu” alisema Dkt.Batilda
Aidha Dkt. Batilda amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha zaidi ya Bilioni 12 kwa ajili ya ukamilishwaji wa miradi ya BOOST inayoendelea kutekelezwa kwa kasi.
Kikao hiki kinahusisha mapitio ya taarifa za utekelezaji wa miradi ya elimu kupitia Program ya BOOST pamoja na maandalizi ya Mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka huu.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa