Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amezindua ofisi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ya Kanda ya Magharibi tarehe 23 Februari 2024 jijini Tabora, ambayo itatoa huduma katika Mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma.
Waziri Bashe amepongeza Benki ya TADB kwa hatua ya kuzidi kupanua wigo wa huduma zenye masharti nafuu na wezeshi kwa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa na kuongeza kuwa upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wakulima, wavuvi na wafugaji, utahamasisha zaidi ukuaji wa biashara katika mnyororo wa thamani kwenye mikoa itakayohudumia.
"Siku ya leo tumepoteza Mwalimu na Kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika sekta ya ushirika hapa nchini, Afrika na Dunia kwa ujumla. Mzee Alhaj Hassan Wakasuvi, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora alikuwa mdau muhimu wa maendeleo katika nyanja za ushirika, hivyo naelekeza tumuenzi kwa kuita ofisi hii ya Kanda ya Magharibi 'Wakasuvi House"" amesema Waziri Bashe.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege ameeleza kuwa ufunguzi wa ofisi hiyo umelenga azma ya benki hiyo kusogeza huduma karibu kwa wakulima ambapo watanufaika na mikopo yenye masharti nafuu, kwa viwango vya riba za chini na kutoa muda mrefu zaidi wa marejesho kwa wakulima ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji ya kuleta mapinduzi katika Sekta ya Kilimo.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege, Bodi na Menejimenti ya TADB. Aidha, Mhe. Balozi Dkt. Batilda amepongeza hatua hiyo muhimu ya kuleta huduma za Benki ya TADB katika Mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma na kueleza kuwa ni ukombozi kwa wakulima, wavuvi na wafugaji katika kukuza mitaji yao.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa