Leo Januari 24, 2024 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ndugu Jumanne Wambura Wagana amekabidhi Magodoro na Madaftari ambayo ni msaada kutoka benki ya CRDB kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Ziba ambayo jana Januari 23, 2024 iliunguliwa na Bweni la Wavulana na kuteketeza vitu vyote ndani ya Bweni.
"Ndugu zangu Viongozi mkiongozwa na Mh. Mkuu wa wilaya, waalimu, Wazazi, wanafunzi ninyi mmekuwa wadau wetu wakubwa hivo lazima tuungane kwenye shida na raha na tulipopata taarifa ya janga hili tuliona tuje kuwapa pole na kuwakabidhi magodoro na madaftari kwani tumeambiwa mmeunguliwa vitu vyote bwenini” alisema Ndugu Wagana
Akipokea Msaada huo kutoka CRDB kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mh. Sauda Mtondoo ameishukuru sana Benki ya CRDB kwa msaada huo wa Magodoro na Madaftari na kuwaomba wadau wengine waendelee kuwashika mkono.
Ikumbukwe, mchana wa Leo Januari 24, 2024 Kampuni ya Ununuzi wa Tumbaku ya ALLIANCE ONE ilimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian Magodoro na Mablanketi arobaini ikiwa ni msaada kwa wanafunzi wa Sekondari Ziba.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa