Mkuu wa Wilaya Urambo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mhe. Elibariki Bajuta ameendelea na ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyoo katika Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari Wilayani Urambo na kujionea maendeleo ya ujenzi wa vyoo hivyo wenye kuridhisha.
Katika ukaguzi huo DC Bajuta leo Februari 14, 2024 amekagua vyoo katika Shule ya Sekondari Imara, na Shule ya Msingi Imalamakoye pamoja na Shule ya Msingi Ndorobo nakupongeza hatua zinazoendelea kuonekana katika ukamishaji wa ujenzi huo.
Aidha ametoa maagizo kwa Waandisi wa Wilaya ya Urambo kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuondoa kasoro ndogondogo zilizojitokeza ili fedha za Serikali na Wafadhili zitumike vyema kupitia miradi mbalimbali ya elimu iliyopo Wilayani Urambo.
Pamoja na ukaguzi huu DC Bajuta amewataka walimu na watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha Watoto wote walioandikishwa wanaripoti kuanza masomo bila kubakiza hata mmoja nyuma ikiwa ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian aliyoyatoa Januari 8, 2024.
DC Bajuta anaendelea na ziara ili yake wilayani Urambo ili kuhakikisha miradi yote inayojengwa na Serikali ya Awamu Ya Sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatumika vizuri kama ilivyokusudiwa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa