Mkuu wa Wilaya ya Urambo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mhe. Elibariki Bajuta amepokea magodoro 80 kutoka kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya JTI iliyopo mkoani Tabora kama msaada wao katika kuboresha Elimu ya Mtoto wa Kike katika Wilaya ya Urambo, Februari 27, 2024.
Magodoro haya yametolewa na Kampuni ya JTI kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kitaifa ya Margaret Sitta.
Kupitia kaulimbiu ya "Mimba kwa mtoto wa kike Urambo haikubaliki, Tumpe Fursa ya kusoma mtoto wa kike kwa maisha yake ya Baadaye" kampuni ya JTI imekuwa miongoni mwa kampuni inayomuunga mkono jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Urambo kuhakikisha changamoto mbalimbali kwenye sekta ya elimu zinapungua wilayani humo. Na ikumbukwe kuwa Urambo ni miongoni mwa wilaya ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukusanya madawati na kuondokana na changamoto ya Watoto kukaa chini.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa