Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu amewataka maafisa nyuki wa Wilaya kuzitumia vizuri pikipiki ambazo wamekabidhiwa leo Septemba 25, 2023, kwenye hafla ya kukabidhi pikipiki mpya 15 zenye thamani ya shilingi milioni 131, fedha kutoka Mradi wa Kuboresha Mnyororo wa Thamani ya Ufugaji Nyuki (BEVAC)
"Nawaelekeza maafisa mnaopewa pikipiki hizi mkazitumie vizuri kwa kuhakikisha zinatumika kutimiza majukumu yaliyopangwa kuboresha shuhuliza za ufugaji nyuki na siyo vinginevyo” alisema DC Mwansasu
DC. Mwansasu ameleza kuwa, Serikali na wadau wake wanatambua mchango na thamani ya shughuli za ufugaji wa Nyuki ambao kila siku umekuwa na tija kubwa kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora.
“Serikali inatambua umuhimu wa shughuli za ufugaji nyuki katika kutoa fursa za kiuchumi kwa wanajamii wengi hasa vijana na wakina mama. Hivyo kupitia pikipiki hizi tunaamini maafisa hawa wataweza kusaidia kuongeza tija ya uzalishaji, uboreshaji wa mnyororo wa thamani na kupelekea kuongezeka kwa mapato katika halmashauri zetu” Alisisitiza Mhe. Mwansasu.
Sambamba na hilo Mhe. Mwansasu ameeleza baadhi ya mabadiliko ambayo yanaendelea kufanyika ili kuhakikisha shughuli za ufugaji wa Nyuki zinakwenda na wakati ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi tofauti na hapo awali.
“Kwa sasa takribani mizinga 560,000 inayotumika na wafugaji katika maendeo yautekelezaji wa mradi ni mizinga ya Asili (84%) na mizinga ya kisasa ni 110,000 tu (16%). Napenda kuyasema haya ambayo ni baadhi tu ya mambo muhimu ya kuzingatia ili kuendana na kasi ya teknologia iliyopo sasa, kwani ufugaji Nyuki wa sasa siyo ule wa mazoea kama walivyokuwa wanafanya mababu zetu”
Kwa miaka ya hivi karibuni Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, shughuli za ufugaji Nyuki hasa kwa Mkoa wa Tabora umehimarika sana na hii ilipelekea Asali kutoa Tabora kupata hati ya utambuzi wa Kitamaifa huko nchini Afrika Kusini. Hali hii imechangia kuhimiza wadau wa shughuli za ufugaji Nyuki kuunga mkono shughuli hizo na kufanya mabadiliko makubwa sana.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa