MKUU wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda amewataka Wazazi kuhakikisha wanawalea watoto wao katika misingi bora ili wasijihusishe na vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na ubakaji.
Alisema hali hiyo itawafanya kuwa na maadii bora na kuwasababishia kujihusisha na shughuli halali za kuwaingizia kipato.
Dkt.Nawanda alitoa kauli hiyo jana wakati wa Mahafali ya saba ya Chuo cha Tabora Polytechnic ambapo wahitimu zaidi 273 walitunikiwa stashahada katika fani za wafanasia, , elimu na malezi ya watoto, uandishi wa habari na utangaaji, utunzaji kumbukumbu, Uongozaji watalii na ukarimu na ukatibu Muhtasi .
“Niwaombe wazazi hao vibaka ni watoto wetu tuendelee kuwakanya na kuwalea katika misingi sahihi…mwisho siku mwisho wa mwizi ni mbaya… na kama umkanyi mtoto wako jamii itakmya itachukua nafasi ambayoutakuja kujitia” alisisitiza.
Aliwataka wazazi kuwaonya watoto wao kuachana na vitendo vya uhalifu vinginevyo watakutana na mkono wa sheria ikiwemo kufikishwa Mahakamani.
Dkt. Nawanda alisema Serikali ipo kwa ajili ya kulinda raia na mali zao na kama watashindwa kutii malezi ya wazazi wao watakuwa wamejiingiza kwenye mkono wa sheria.
Aidha aliwataka wazazi kuendelea katika uwekezaji katika elimu ya watoto wao ili hatimaye waweze kuwa wananchi wazuri ambao watashiriki katika ujenzi wa Taifa.
Dkt. Nawanda alisema uwekezaji wa elimu kwa watoto wao utasaidia kuwaondoa katika uhalifu na kufikiria zaidi katika shuighuli halali za maendeleo.
Alisema wataimarisha doria za usiku katika maeneo yote na Wilaya ya Tabora na kutengeza Polisi Jamii kwa lengo la kuwahakikishia wakazi wa Wilaya hiyo usalama wao na mali zao.
Dkt. Nawanda alisema tatizo la uhalifu litakomesha ili wananchi waweze kufanya shughuli zao halali bila hofu yoyote.
Awali Mkurugenzi wa Chuo hicho Shabani Mrutu alimeiomba Mkuu wa Wilaya kuwasaidia kukabiliana na tatizo la wizi na ukabaji unaofanywa na baadhi ya vijana wasio waadilifu katika eneo hilo nyakati za usiku.Alisema tatizo hilo limekuwa likisbabisha usumbufu kwa jumuiya ya wanachuo na watumishi kwa ujumla
Alisema changamoto nyingine inayokikabili chuo hicho ubovu wa kipande cha barabara kutoka barabara kuu kuelekea Chuoni.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa