Leo Juni 6,2023 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amehutubia Viongozi, Wakufunzi, Walimu, Wanafunzi a Wananchi mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA a UMISSETA yanayofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.
Ambapo sehemu kubwa ya hotuba yake amesisitiza suala la michezo mashuleni kwa kuhakikisha vipindi vya michezo vinazingatiwa. Sambamba na utengaji na matumizi sahihi wa maeneo kwa ajili ya michezo mashuleni. Na pia kwenye kila shule pawepo na walimu/ mwalimu wa michezo ili kuhakikisha suala la michezo linatekelezeka.
Dkt Philip Mpango amewataka wadau wa sekta ya michezo, Wizara ya Mambo ya Nje kutafuta fursa nje ya mipaka ya Tanzania ili kuhakikisha watoto wenye vipaji wanapata fursa ya ufadhili na kuendeleza vipaji vyao.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa