Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amezitaka mamlaka zote zinazohusika na usimamizi wa hidadhi kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji kutenga na kubainisha maeneo kwa ajili ya malisho ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira pamoja na uvunjifu wa amani. Ameyasema hayo leo Obtoba 6, 2023 alipotembelea hifadhi ya Uyumbu, Wilayani Urambo.
“Napenda nitoe wito kwa mamlaka zote zinazosimamia uhifadhi wa mazingira kuhakikisha zinashirikiana na watendaji wa kata na vijiji kutenga maeneo kwa ajili ya malisho ili kuepukana na uharibivu wa mazingira na uvunjifu wa Amani kwenye maeneo ya hifadhi”
Akijionea uharibifu wa mazingira ulifanywa na baadhi ya wananchi kwenye hifadhi ya Uyumbu, Mhe. Mkuu wa Mkoa, ameliagiza Jeshi la Polisi na TFS Wilayani Urambo kuwakamata wote wanahusika na uuzaji wa maeneo yalio kenye hifadhi.
“Naliagiza jeshi la Polisi kukamata wote waliohusika na uuzwaji wa maeneo yalio kwenye hifadhi na ikiwezekana warudishe fedha kwa waliowauzia”
Katika ziara yake hiyo, Mkuu wa Mkoa Dkt. Batilda ameeleza dhima kubwa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika suala zima La uhifadhi wa mazingira kwa kuhakikisha kila Mkoa
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa