Julai 13, 2023, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian ametembele Wilayani Nzega kwa ajili ya ukaguzi miradi mbalimbali ya maendeleo hususani miradi ya ujenzi wa shule zinazojengwa na kuboreshwa kupitia Programu ya BOOST.
Kupitia Program ya BOOST, Mkoa wa Tabora umepata jumla ya shilingi Bilioni 12.1 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi mpya 17, vyumba vya madarasa 118, vyumba vya madarasa ya mfano ya Elimu ya Awali 16, matundu ya vyoo 130 na nyumba za walimu 2 (2 in 1). Ambapo Nzega DC imepata jumla ya shilingi Bilioni 1.4 na Nzega TC imepata jumla ya shilingi Bilioni 0.98.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa