• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

JAFO ATAKA KUONDOLEWA KWA VIKWAZO KWA VIJANA WENYE UFAULU WA CHINI KUENDELEA NA MASOMO

Posted on: March 11th, 2019


JAFO ATAKA KUONDOLEWA KWA VIKWAZO KWA VIJANA WENYE UFAULU WA CHINI KUENDELEA NA MASOMO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo imezitaka Taasisi zinazosimamia mifumo ya elimu kutoweka vikwazo na masharti magumu kwa vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbali mbali.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua Kitaifa Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya Mfumo rasmi wa Elimu (IPOSA). 

Jafo alisema kuwakwamisha vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbalimbali kwa vigezo vya kuwa na ufaulu wa chini ni kuwanyima vijana haki ya kupata ujuzi. 

“Tuache kuweka mifumo yenye roho mbaya inayokwamisha  vijana kielimu na ndoto zao za kishiriki uchumi wa viwanda” alisema.

Jafo alisema kuwa wapo watalaamu wanakaa Ofisini na kuweka vigezo ambavyo vinalenga kukwamisha vijana kuendelea na mafunzo yakiwemo ya ufundi na kuwafanya kushindwa kushirikia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda

Waziri Jafo aliitaka Taasisi ya Elimu ya watu Wazima kuweka mpango kwa vijana ili waweze kuendelea na vyuo vya juu ili taifa liweze kuwa na wataalam wengi.

Kuhusu Mpango wa Elimu Changamani ( IPOSA) alisema umekuja kujibu kauli ya utekelezaji wa uchumi wa viwanda kwani unajengwa na vijana wenye Maarifa.

Waziri  Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa nane na wilaya zake ambako mpango wa IPOSA  unatekelezwa kusimamia ipasavyo na baadae uweze kuenea nchi nzima kama ilivyokusudiwa.

Alisema utekelezaji wa Mpango wa IPOSA usiwe wa zimamoto bali uwe endelevu ili vijana wanufaika waweze kushiriki katika ujenzi wa  maendeleo ya Taifa.

 

Jafo aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutoa fedha kila mwezi kwa ajili ya kugharamia watoto wa kitanzania kupata elimu bila malipo.

Alisema jumla ya shilingi bilioni 23.8 zinatolewa kila mwezi kwa ajili ya kugharamia wanafunzi kusoma bila mzazi kulipa ada na kuwataka watoto kutumia fursa hiyo kusoma kupitia mfumo rasmi.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Tixon Nzunda alisema Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi unatekelezwa kwa majaribio mikoa nane hapa nchini.

Alitaja mikoa hiyo ni Kigoma, Tabora, Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe na Dodoma.

Nzunda alisema mpango wa IPOSA awamu ya kwanza  unatarajia kuwanufaisha vijana wapatao 10,000 kati ya vijana milioni 3.5 waliopo nje ya mfumo rasmi wa elimu.

Alisema Ofisi ya TAMISEMI kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo kama vile UNICEF walitembelea na kubaini vituo 72 vitakavyotekeleza mradi huo katika mikoa hiyo.

 Kwa upande wa Mratibu wa Mpango huo Dkt. Sempheo Siafu alisema kuwa mpango huo utachukua miezi 20 hadi kukamilika huku ufundishaji ukifanyika kwa njia ya nadharia na vitendo ukiwahusisha vijana wenye umri wa miaka 14 hadi 17.

Alisema lengo kuu la mpango huu ni kuhakikisha kuwa na vijana walioelimika, wenye maarifa, ujuzi na stadi za kuweza kuchangia kwa haraka maendeleo ya taifa na kuhimili ushindani.

 

MWISHO.


Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa