• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

JTI YATUMIA MILIONI 20.1 KURUDISHA KWA JAMII

Posted on: November 21st, 2023

Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya JTI imegawa vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 20.1 kwa Watu Wenye Mahitaji Maalumu, Vijana na Wakina mama wafugaji wa nyuki kama sehemu ya kurudisha faida kwa jamii na kuiunga mkono Serikali kwa kutoa misaada kwenye jamii. 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye mazungumzo mafupi na  Makamu Mwenyekiti ya Bodi ya Tumbaku Ndugu Hassan Wakasuvi, Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Anna Makinda, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania Ndugu. Takashi Araki-San na wajumbe wengine kutoka Kampuni ya JTI walioambatana na wageni hao, Novemba 21, 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti ya Bodi ya Tumbaku Ndugu Hassan Wakasuvi, Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Anna Makinda, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania Ndugu. Takashi Araki-San na wajumbe wengine kutoka Kampuni ya JTI walioambatana na wageni hao mara baada ya kufanya mazungumzo mafupi ofisini hapo, Novemba 21, 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania Ndugu. Takashi Araki-San akitoa salamu za kampuni ambapo sehemu Kubwa ya salamu zake ameelezea mchango mkubwa wa Wakulima wa Tumbaku kutoka Mkoa wa Tabora kwenye kukuza uzalishaji katika kiwanda cha Sigara Novemba 21, 2023.

Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Leaf Anna Makinda akitoa salamu za Kampuni ya Ununuzi wa Tumbaku JTI, ambapo sehemu kubwa ya salamu zake ameelezea machango mkubwa wa serikali katika kuwawezesha wakulima ambao pia wamekuwa na mchango mkubwa kwenye sekta ya Kilimo na Kampuni ya JTI Leaf kwa ujumla.

Makamu Mwenyekiti ya Bodi ya Tumbaku Ndugu Hassan Wakasuvi akitoa salamu kutoka Bodi ya Tumbaku ambapo sehemu salamu zake ameelezea maendeleo makubwa yaliofanywa na Serikali katika kuendeleza Kilimo cha Tumbaku hususani Mkoani Tabora na kutoa wito kwa Kampuni ya Tumbaku ya JTI Leaf kuwekeza kwenye miundombinu ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akihutubia baadhi ya wajumbe kutoka kampuni ya JTI, Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora, wadau wa  sekta ya ufungaji wa Nyuki,na wawakilishi kutoka vyama vya watu wenye mahitaji maalumu, Novemba 21, 2023.

Katika hotuba yeke, Mhe. Mkuu wa Mkoa ameeleza mafanikio makubwa yaliofanywa na Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kwa mwaka 2022/2023 mkoa umepata jumla ya tani 8 za mbolea ya ruzuku yenye thamani ya  shilingi Bilioni 19.5, ambapo mpaka sasa tayari wakulima wameshapata Shilingi Bilioni 10.9.

Aidha Mhe. Batilda ameeleza kuwa, mpaka sasa mkoa umepokea Pikipiki 240, Vishikwambi 7 na Soil Scanners 7 kutoka Wizara ya Kilimo ambavyo vinechangia pakubwa kwenye Sekta ya Kilimo Mkoani Tabora.

Pia, kupitia uwekezaji ulofanywa na Serikali, Mkoa wa Tabora umefanikiwa  kuongeza Mapato ya wakulima kutoka Dola Marekani 54 mpaka kufikia Dola za Kimarekani 144.7 na kuchangia ongezeko la Mapato ya Serikali kwa kiasi kikubwa.

Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Anna Makinda akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian vifaa vya watu wenye mahitaji maalumu vikiwemo magongo ya kiwiko jozi 50, magongo ya makwapani jozi 48, baskeli za maguludumu (miguu) matatu 2 na mguu wa bandia Mmoja (1) vyenye thamani ya Shilingi Milioni 11.1. Na kishA Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amemkabidhi mwakilishi wa watu wa wenye mahitaji maalumu vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 11.1, Novemba 21, 2023.

Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Leaf Anna Makinda akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian vifaa vya ufugaji wa vyuki vikiwemo mavazi ya kujikinga na nyuki 20, Mashine za kukamulia asali 20, vifoka moshi 20, visu vya kuvunia asali 20, vifaa vya kukagua na kufungua mzinga wa nyuki 20, vifaa vya kusafishia mizinga 20 na vifaa vya kuchujia asali vitano (5) vyenye thamani ya Shilingi Milioni 9.8. Na kisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amekabidhi vifaa hivyo kwa vijana na wakina mama wanaojihusisha na shughuli za ufugaji wa Nyuki Mkoani Tabora, 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti ya Bodi ya Tumbaku Ndugu Hassan Wakasuvi, Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Anna Makinda, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania Ndugu. Takashi Araki-San na baadhi ya wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya watu wenye mahitaji maalumu mara baada ya zoezi la makabidhiano ya vifaa vya watu wenye mahitaji maalumu na ufugaji wa Nyuki kukamilika, Novemba 21, 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti ya Bodi ya Tumbaku Ndugu Hassan Wakasuvi, Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Anna Makinda, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania Ndugu. Takashi Araki-San na baadhi ya wawakilishi kutoka vikundi vya vijana na wakina mama wafugaji wa Nyuki na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora mara baada ya zoezi la makabidhiano ya vifaa vya watu wenye mahitaji maalumu na ufugaji wa Nyuki kukamilika, Novemba 21, 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti ya Bodi ya Tumbaku Ndugu Hassan Wakasuvi, Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Anna Makinda, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania Ndugu. Takashi Araki-San na baadhi ya wawakilishi kutoka Kampuni ya JTI, mara baada ya zoezi la makabidhiano ya vifaa vya watu wenye mahitaji maalumu na ufugaji wa Nyuki kukamilika, Novemba 21, 2023.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti ya Bodi ya Tumbaku Ndugu Hassan Wakasuvi, Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Anna Makinda, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania Ndugu. Takashi Araki-San na baadhi ya waandishi wa habari kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa Tabora mara baada ya zoezi la makabidhiano ya vifaa vya watu wenye mahitaji maalumu na ufugaji wa Nyuki kukamilika, Novemba 21, 2023.



Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • WIZARA YA AFYA NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TABORA YAENDESHA KIKAO ELEKEZI CHA MREJESHO WA MAFUNZO NA MAPITIO YA AFYA YA MAMA NA MTOTO.

    May 14, 2025
  • JESHI LA POLISI TABORA LAPATA MAGARI 6 MAPYA KWA AJILI YA KUIMARISHA USALAMA WA RAIA

    May 12, 2025
  • BODI YA WADHAMINI MFUKO WA MISITU TANZANIA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO TABORA.

    May 07, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa