Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imetembelea mradi wa ukarabati wa Makazi ya Wazee yaliyopo puli Mkoa wa Tabora leo tarehe 12 Machi, 2024 na kueleza kuridhishwa na maboresho yaliyofanyika ikiwemo ujenzi wa jengo jipya.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Fatma Hassan Toufia imepongeza jitihada zilizochukuliwa na Serikali chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan za kukarabati makazi ya Wazee hao hasa ya ujenzi wa jengo jipya ambalo litawasaidia wazee wanaoishi hapo kupata sehemu bora pakuhishi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamil, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis imeihakikishia Kamati hiyo kuwa serikali itahakikisha inakamilisha kila kitu ambacho ni muhimu katika makazi hayo kwa ajili ya ustawi bora wa wazee wanaoishi hapo.
Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ipo katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kesho inatarajiwa kuelekea Mkoani Mara kwa ajili ya kazi hiyo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa