Katibu Mkuu wa CCM Ndugu. Daniel Chongolo amempongeza Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa kutoa fedha ambazo zimetumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo Ikiwemo Maji na Elimu Mkoani Tabora. Ametoa pongezi hizo leo Julai 23, 2023 alipokuwa akitoa hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Kanda ya Kati (Tabora, Singida na Dodoma).
Pia ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa kusimamia vema miradi ya elimu na kufanikisha Mkoa Kupokea Idadi kubwa ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka elfu mbili (2000) hadi elfu sita (6000) kwa mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa, Kupitia llani ya CCM ya mwaka 2020 imetoa dira va namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma ya Maji Safi na Salama kwa Wakazi waishio Mijini kwa asilimia 95, na Vijiji kwa asilimia 85 mpaka kufikia mwaka 2025. Ambapo Mkoa wa Tabora kupitia Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) ulipata Jumla ya Shilingi Bilioni 35.98.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa