Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Mhe. Abdulrahman Kinana ameridhishwa na taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa muda wa miezi sita ambayo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian aliiwasilisha leo Julai 30, 2023 kwenye Ukumbi mdogo wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Tabora.
Aidha, Mhe, Kinana amewataka viongozi wa Serikali kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa kikamilify kwani ndio watendaji wakuu wa Serikali ambao wanasimamia utekelezaji wote wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020.
Ikumbukwe kuwa, mnamo Julai 21,2023 Mkuu wa Mkoa aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Tabora ambayo wajumbe walimpongeza na waliikubali taarifa hiyo kwa asilimia mia moja.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa