Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu amefungua ramsi Maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa Reli yatakayofanyika katika viwanja vya Chuo Cha Reli, Manispaa ya Tabora.Oktoba 9, 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akisalimiana na baadhi ya viongozi kutoka kwenye mashirika mbalimbali ya usafirishaji kwa njia ya reli yakiwemo TRC na TAZARA ambayo yamehudhuria kwenye maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa Reli.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akitembelea na kupata maelezo kutoka kwa mmoja ya watendaji kutoka Wizara ya Uchukuzi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa Reli.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya watendaji wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) na kujione baadhi ya shughuli ambazo zinafanywa na Chuo hiko, kikiwa kama miongoni wa wadau wakubwa kwenye sekta ya usafirishaji.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akishuhudia moja ya majaribio ya mfumo wa ulinzi katika reli, ambao umebuniwa na wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT).
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, ambapo alipata nafasi ya kujionesha vifaa mbalimbali ambavyo vitatumika kwenye Uzimaji wa Moto na Uokoaji.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akitembelea banda la Mamlaka ya Heri ya Hewa Tanzania (TMA) na kupata maelezo ya kima namna TMA inavyoshirikiana na mashirika ya TRC na TAZARA kwenye suala zima la Usalama wa Reli.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akipata maelezo kutoka Jeshi la Polisi kitengo cha Usalam Barabarani, na kujionea baadhi ya vifaa ambavyo vinatumika kwenye masuala ya Usalama. Usalama wa Reli unategemea sana usalama wa barabarani ambao unasimamiwa na Jeshi la Polisi kwa asilimia kubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akisalimiana na baadhi ya vijana waendesha pikipiki (Bodaboda) ambao wamepitia mafunzo ya Usalama Barabarani na kupatia vyeti.
Maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani wa Reli yanafanyika hapa Mkoani Tabora kwenye Viwanja vya Chuo Cha Reli, Manispaa ya Tabora. Yameanza leo Oktoba 9, 2023 na kufikia tamati Oktoba 9, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa