• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MAAFISA USTAWI WA JAMII WAPEWA MAFUNZO YA UPANGAJI WA MIPANGO NA BAJETI YA SHUGHURI ZA USTAWI WA JAMII

Posted on: January 31st, 2024

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imesema itawekeza katika kuhakikisha   maafisa ustawi wa jamii katika halamshauri zote nchini wanapatiwa mafunzo ili kuwajengea maafisa hao uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kuhudumia wananchi.

Hayo yamesemwa leo Januari 31, 2024 Mkoani Tabora na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Ismail Kaponta wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya upangaji wa mipango na bajeti ya shughiri za ustawi wa jamii uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Grand Penta, Manispaa ya Tabora.

 Akitoa  hotuba yake Dkt. Kaponta  amesema kuwa mafunzo haya yana malengo ya kuwajengea uwezo maafisa ustawi wa jamii katika kutimiza majukumu yao hususani katika upangaji wa mipango na bajeti ambayo itasaidia kukamilisha adhma ya serikali katika kuhakikisha huduma za ustawi zinawafikia.

“Nipende kukumbushia kuwa malengo ya mafunzo haya ni kuwajengea uwezo nyinyi maafisa ustawi wa jamii ambao unakwenda kuwahudumia wananchi kwenye halmashauri zenu hususani kwenye upangaji wa mipango kwa kuzingatia bajeti” alisema Dkt. Kaponta

Aidha Dkt. Kaponta amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii kote nchini kusimamia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo  kwa kuzingatia sheria na miongozo inayopaswa kufuatwa katika kutoa huduma za ustawi wa jamii kwa jamii ili kupunguza matatizo yanayoweza kutokea kutokana kwenye jamii hizo.


Naye Mratibu wa Mipango na Bajeti Shughuri za Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI Bi. Zainabu Kitembe amekiri kuwepo na changamoto ya ufinyu wa bajeti kwa maafisa ustawi wa jamii katika kukamilisha majukumu yao ya kila siku jambo ambalo upelekea maafisa wengi kufanya kazi kwenye mazingira magumu.

“unakuta kuna wakati maafisa wa ustawi wa jamii wanafanya kazi kwa “stress” sana na wengi wao hawana furaha na kazi yao kutokana na kukosekana kwa bajeti ya kutekeleza majuku yao ya kuhudumia jamii” alisema Bi. Zainabu 

 

Ameongeza kuwa, licha ya kuwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti, bado serikali imeendelea kutambua mchango na nafasi ya maafisa hao kwenye ustawi wa jamii na sasa imetoa nafasi kwa maafisa hao kupata mafunzo haya ya upangaji wa mipango na bajeti ya shughuri ya ustawi wa jamii. 

“tunatambua mchango wenu kwenye ustawi wa jamii, na tulitamani maafisa wote wa ustawi wa jamii wahudhurie mafunzo haya lakini kutokana na bajeti mmekuja wachache” aliongeza Bi. Zainabu.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Shirika la PACT Tanzania Bi. Flora Nyagawa amesema kuwa, PACT imetoa mchango mkubwa wa uanzishwaji wa mafunzo ya mfumo wa upangaji wa mipango na bajeti ya ustawi wa jamii na sasa hivi wameendelea kufadhiri mafunzo haya kwa maafista wa ustawi wa jamii na watalaamu wengine wanahusika na shughuri za ustwawi wa jamii.

Mafunzo haya ya mfumo wa upangaji wa mipango na bajeti ya shughuri za ustawi wa jamii yalioanza Januari 29, 2024, yanahusisha maafisa ustawi wa jamii, maafisa mipango, waganga wakuu na makatibu wa afya kutoka halmashauri mbalimbali nchini.yamefadhiliwa na shirika la kimataifa la PACT Tanzania kupitia mradi wake wa ARCHIVE unaohusika na kusaidia Watoto wanaoishi mazingira hatarishi.

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa