Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Deusdedith Katwale amehitimisha mafunzo ya utengenezaji wa nyuzi na vitambaa kwa kutumia teknolojia ya Indonesia ambayo yalidumu kwa muda wa siku kumi na nne (14) yakihusisha walimu wawili kutoka nchini Indonesia na wanafunzi ishirini na tano (25) kutoka mkoani Tabora leo Machi 15, 2024.
Mhe. Katwale amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwaunga mkono vijana hao 25 ambao wamemaliza mafunzo hayo kwa kuwapatia mikopo na vifaa mbalimbali ili kuwawezesha vijana hao kutumia ujunzi wao kuzalisha bidhaa mbalimbali zitokanazo na pamba.
Sambamba na hilo, Mhe. Katwale ametoa wito kwa watendaji wa halmashauri za mkoa wa Tabora kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri na wezeshi kwa vijana hao kutumia ujunzi walioupata kwa kufanya shughuri mbalimbali za uzalishaji.
Naye mkufunzi kutoka Indonesia Bi. Venny Alamsyah ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kutoa fedha ambazo zimesaidia wanafunzi hao kupata mafunzo hayo ambayo ya yanakwenda kubadilisha maisha yao.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Cha VETA Tabora Dkt. Zebedayo Kyomo ameshukuru kwa mafunzo hayo kufanyika katika chuo hiko na kwamba kupitia mafunzo hayo wapo wanafunzi kutoka chuo hiko ambao wamefaidika moja kwa moja na uwepo wa mafunzo hayo.
Ikumbukwe kuwa, mafunzo haya yalifunguliwa mnamo Machi 4, 2024 na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akishirikiana na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Tri Yogo Jatmiko
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa