Kutoka Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameshawasili viwanjani hapo na kuungana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tabora pamoja na Wananchi kwa ajili ya kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Mkoani Tabora kuanzia Leo Septemba 14, 2023 Ukitokea Mkoani Mbeya na unatarajiwa kumaliza mbio zake Septemba 21, 2023 ambapo utakabidhiwa Mkoani Singida.
Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingura, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa"
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa