Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo Manispaa ya Tabora, kwa ajili ya kukabidhi zawadi ya Krismass na Mwaka Mpya kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa watoto waliozaliwa usiku wa kuamkia leo Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akipata taarifa na maelezo kwa ufupi kuhusiana na watoto waliozaliwa usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuwasili Hospitalini hapo kwa ajili ya kukabidhi zawadi ya Krisimass na Mwaka Mpya kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa watoto waliozaliwa usiku wa kuamkia leo Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akiongea na baadhi ya wakina mama waliojifungua usiku wa kuamkia Leo Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akimbeba mmoja kati ya watoto Ishirini na tatu (23) waliozaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete, Januari 1, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akikabidhi zawadi ya Krissmas na Mwaka Mpya kwa wakina mama waliojifungua usiku wa kuamkia leo, mara kuwasili katika hospitali ya Rufaa ya Kitete, Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akiagana na baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kitete mara baada ya zoezi la kutoa zawadi ya Krissmas na Mwaka Mpya kwa watoto waliozaliwa usiku wa kumkia leo Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akiwasili katika kituo cha kulelea watoto Yatima na wasiojiweza Igambilo kilichopo Kata ya Misha kwa ajili ya kukabidhi zawadi ya Krisimass na Mwaka Mpya kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa watoto yatima na wasiojiweza leo Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akipata taarifa na maelezo mafupi kuhusiana na kituo cha kulelea watoto Yatima na wasiojiweza Igambilo mara baada ya kuwasili kituoni hapo kwa ajili ya kukabidhi zawadi ya Krisimass na Mwaka Mpya kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa watoto yatima na wasiojiweza leo Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akiongea na kutoa salamu za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa watoto Yatima na wasiojiweza waliopo katika kituo cha Igombelo, kabla ya kukabidhi zawadi ya Krismass na Mwaka Mpya kwa watoto hao leo Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akikabidhi zawadi ya Krismass na Mwaka Mpya kwa watoto Yatima na Wasiojiweza waliopo katika kituo cha Igombelo, zawadi kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Januari 1, 2024.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Wasiojiweza Ndugu. Halima Malaswai akitoa neno la Shukrani kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian kukabidhi zawad ya Krismass na Mwaka Mpya kituoni hapo Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akiwa na watoto Yatima na Wasiojiweza wakiliombea taifa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya zoezi la kukabidhi zawadi ya Krismass na Mwaka Mpya kukamilika, Januari 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian akiagana na baadhi ya viongozi wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Igombelo mara baada ya zoezi la kukabidhi zawadi ya Krismass na Mwaka Mpya kumalizika leo Januari 1, 2024.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa