Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwasili katika makao makuu ya Jimbo Kuu Katoliki Tabora kwa ajili ya kukutana na Mwadhama Antonio Kardinali Tagle, Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa Watu, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora na Askofu Angelo Accattino, Balozi wa Vatcan nchini Tanzania , Novemba 18, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akisalimiana na Mwadhama Antonio Kardinali Tagle, Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa Watu na Askofu Angelo Accattino, Balozi wa Vatcan nchini Tanzania mara baada ya kuwasili Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Novemba 18, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Novemba 18, 2023.
Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora akifanya zoezi la utambulisho wa wageni mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kuwasili Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Novemba 18, 2023.
Kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akitoa salamu za Serikali kwa Mwadhama Antonio Kardinali Tagle, Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa Watu, Novemba 18, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akikabidhi zawadi ya mishumaa Mwadhama Antonio Kardinali Tagle, Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa Watu, Novemba 18, 2023.
Mwadhama Antonio Kardinali Tagle, Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa Watu akifurahia zawadi ya mishumaa na kikapu kilichotengenzwa Mkoani Tabora, Novemba 18, 2023.
Ameonekana kuvutiwa na kuipenda zawadi hiyo ya Kikapu kutoka Tabora na kuhaidi kwenda kumpatia mama yake mzazi kama ishara ya kukubali na kufurahishwa na ubunifu huo.
Pia, Mwadhama Antonio Kardinali Tagle amevutiwa na mkakati wa Serikali ya Tanzania kuhamasisha utalii wa Ndani na shughuli za ufugaji wa nyuki Mkoani Tabora.
Mwadhama Antonio Kardinali Tagle, Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa Watu na Askofu Angelo Accattino, Balozi wa Vatcan nchini Tanzania wakifurahia mara baada ya kusoma kitabu kwa lugha ya kiswahili. Wageni hao wameonekana kuvutiwa sana na lugha ya kiswahili kwa kijifunza maneno machache, Novemba 18, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akielezea kwa ufupi Mkoa wa Tabora hususani miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa hususani mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa SGR, kutoka Dar Es Salaam mpaka Tabora, na Kutoka Tabora mpaka Kigoma na Mwanza. Ambapo Wageni hao wameonesha kuvutiwa sana na kasi ya maendeleo nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Antonio Kardinali Tagle, Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa Watu, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora na Askofu Angelo Accattino, Balozi wa Vatcan nchini Tanzania, mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo mafupi katika ofisi za Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Novemba 18, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiagana na Antonio Kardinali Tagle, Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa Watu mara baada ya kutana na kufanya mazungumzo mafupi katika ofisi za Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Novemba 18, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa