Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha, amewaongoza mamia yawaombolezaji katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoawa Tabora, Marehemu Panini Kerika nyumbani kwake Ipuli, Mnarani.
Katika ibada ya kumuaga marehemu, Baba ParokoPadri Pascal Kitambi wa Parokia ya Ipuli alisema kuwa maisha hayaishi kwasababu ya kifo, bali huendelea kupitia matendo yetu. Alisisitiza kuwa,"Tujifunze ili tukapoondoka hapa duniani, tuache jina na matendo ambayoyatafuatana na sisi," alieleza Padri Kitambi.
Akitoa salamu za pole kwa waombolezaji, Mhe.Chacha aliwataka ndugu, jamaa, na marafiki wa marehemu kumtunza mjanealiyeachwa ili aweze kumudu kuwalea watoto wake kwa amani na utulivu.Vilevilealiwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa Baba Askofu Kardinali ProtaseRugwambwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima kwa familia ya marehemu. Viongozi hao walitoa polenyingi kwa familia, jamaa, na marafiki wa marehemu.
Mwiliwa Marehemu Panini Kerika umeondoka leo kuelekea nyumbani kwake Mto wa Mbu,Jijini Arusha, na utazikwa siku ya Jumamosi, Februari 22, katika kijiji kwaoNgorongoro. "Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe."
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa