Mhe. Methew amebainisha kuwa, katika juhudi za kuhimarisha huduma ya mawasiliano, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepanga kujenga minara mia saba hamsini na nane (758) katika wilaya mia moja na thelathini na tisa (139) na tayari Serikali imeshatenga fedha zaidi ya Bilioni 129 sawa na asilimia 40% ya mradi huo.
Sambamba na hilo Mhe. Naibu Waziri ameweka wazi mikakati ya Serikali ya kuhakikisha elimu ya kompyuta inaanzia kutolewa katika ngazi ya chini badala ya kusubiri katika ngazi za elimua ya juu. Na mpaka sasa tayari Serikali imeshatia mkazo somo la kompyuta mashuleni hususani shule za msingi na sekondari ili kuhakikusha huduma za masiliano zinakuwa na tija kwa jamii.
Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, ameeleza kuwa, Mkoa wa Tabora unatambua kazi Kubwa inayofanywa na Mhe. Rais na kwamba ukamilishwaji wa huduma za mawasiliano zitasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa mkoa na Tanzania kwa Ujumla.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Kundo A Methew alikuwa na ziara ya siku moja Mkoani Tabora, ambapo alikagua miradi mitatu ya ujenzi wa minara ya mawasiliano iliyopo wilayani Nzega na kisha kuelekea Mkoani Shinyanga.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa