Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Paul Matiko Chacha amekutana na kufanya mazungumzo na kamati ya mahusiano ya dini mbalimbali mkoa wa Tabora iliyoongozwa na baba Askofu Dkt. Elias Chakupewa,askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tabora katika ukumbi mdogo wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora.
Akiitambulisha kamati hiyo Askofu Elias Chakupewa ambaye pia ndio mwenyekiti wa kamati hiyo amesema wamefika ofisi ya mkuu wa mkoa kwa lengo kuu moja kujitambulisha na kuomba ushirikiano wa kufanya kazi pamoja katika kujenga umoja,Amani na mshikamano katika mkoa wa Tabora.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha ameishukuru kamati hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ikiwa ni pamoja na kusimamia maadili mema katika jamii kupitia mafundisho ya dini mbalimbali yanatolewa na viongozi hao.Amewaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kutimiza majukumu yao,lakini pia ameahidi kuwapatia msaada wa kila hali ili kufanikisha azma ya kulinda na kudumisha Amani ya taifa letu.
Kamati ya mahusiano ya dini mbalimbali mkoa wa Tabora inajihusisha na usimamizi wa mahusiano kupitia dini,kuelimisha jamii kupitia dini pamoja na kusimamia Amani na utulivu kati ya dini mbalimbali.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa