• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MKUU WA MKOA WA TABORA, MHE. DKT PHILEMON SENGATI AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

Posted on: May 4th, 2021

TAARIFA KWA UMMA (PRESS RELEASE) YA

MKUU WA MKOA WA TABORA, MHE. DKT PHILEMON SENGATI

KWA WAANDISHI WA HABARI WA TABORA – TAREHE 04/05/2021,

KUHUSU UZINDUZI WA MWONGOZO WA UWEKEZAJI WA MKOA UTAKAOFANYIKA TAREHE 08 MEI 2021 – 

KATIKA UKUMBI WA MTEMI ISIKE MWANAKIYUNGI

 

Ndugu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora,

Ndugu Wakuu wa Sehemu na Vitengo Sekretarieti ya Mkoa,

Ndugu zangu Wanahabari, 

Mabibi na Mabwana.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Kazi iendelee)

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana hapa leo kwa lengo la kuwaeleza kuhusu tukio muhimu litakalofanyika Mkoani kwetu tarehe 08/05/2021.

 

Ndugu Waandishi wa Habari,

Nichukue nafasi hii kuwataarifu kwamba Mkoa wa Tabora utazindua rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Tabora tarehe 08/05/2021 katika Ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi, uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo, Mgeni Rasmi wa tukio hilo atakuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey I. Mwambe (Mb).

Ndugu Wanahabari, kwa kuwa ninyi ni wadau muhimu wa maendeleo katika Mkoa wetu, nimeona kuwa ni vema niwaite hapa ili niwafahamishe kuhusu tukio hilo muhimu kwa uchumi wa Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla ili nanyi kwa kutumia taaluma yenu mtangaze na kuwahabarisha wananchi wa Mkoa wa Tabora, na Watanzania wote kufuatilia kwa karibu tukio hilo katika vyombo vya habari.

Ndugu Wanahabari, nichukue fursa hii tena, kuwaeleza kwa kifupi umuhimu wa Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Tabora. Mwongozo huu unaeleza fursa muhimu zilizopo Tabora ili kumrahisishia mwekezaji kufanya maamuzi ya kuwekeza Tabora, na utamsaidia mwananchi kufahamu jinsi ya kufaidika na uwekezaji tarajiwa. Maeneo muhimu yaliyoainishwa kwenye kitabu cha mwongozo wa uwekezaji ni pamoja na;

Hali ya kijiografia, kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutawala ya Mkoa.

Sababu za kuwekeza Tabora.

Huduma wezeshi zilizopo kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na nje ya Mkoa.

Maeneo ya kupaumbele ya kuwekeza katika Mkoa.

Miundombinu wezeshi iliyopo.

Orodha ya taasisi wezeshi zilizopo kwa ajili ya kurahisisha uwekezaji.

Orodha na ukubwa wa Ardhi iliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji mbali mbali na,

Uwepo wa Mawasiliano muhimu (simu & barua pepe) kwa ajili ya kutolea ufafanuzi wawekezaji.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Kauli Mbiu ya Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Tabora ni:        “ Wekeza Tabora kwa Uchumi wa Kijani “  Maana ya kauli mbiu hii ni kuueleza umma kuwa Msingi mkuu wa uchumi wa Tabora unategemea uzalishaji wa malighafi zinazotokana na kilimo, mifugo na maliasili. Hivyo, ni muda muafaka sasa kwa Wananchi wetu kujiandaa na kuzitumia kikamilifu fursa na vivutio vilivyoainishwa katika Mwongozo huo ili kuvutia uwekezaji. 

Na kama mnavyofahamu kuwa mnamo 01 Julai, 2020 Nchi yetu iliingia katika uchumi wa kati ambao msingi wake mkuu ni viwanda. Hivyo, nawaomba wananchi wote wa Tanzania kutumia fursa hii kuchangamkia fursa na vivutio vilivyopo katika Mkoa wa Tabora ili kujenga viwanda vya kuchakata na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na kilimo, mifugo, nyuki, madini na maliasili zingine.

Ndugu Wanahabari, hadi kufikia tarehe ya leo, maandalizi ya uzinduzi yanaendelea vizuri, ambapo tumealika wawekezaji wakubwa wa ndani wakiwemo Mohamed Enterprises (MeTL), Azania Group, Bakhresa Group, Kahama Oil Mills na Jambo Group of Companies. Tumewaalika wawekezaji hao ili waje waone fursa zilizopo katika Mkoa wetu na namna watakavyozitumia kufanya uwekezaji mkubwa.

 

Ndugu Wanahabari,

Ni matarajio yangu kuwa mtausaidia Mkoa wa Tabora kwa kupitia vyombo vya habari kutangaza, kutoa elimu na kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa Mwongozo wa Uwekezaji ambao utaingizwa katika tovuti ya Mkoa mara baada ya uzinduzi.

 

WITO WANGU KWA WANANCHI; 

Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Tabora, taifa kwa ujumla na nchi jirani kujipatia nakala ya kitabu cha mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa ambacho kitapatikana bure katika tovuti ya Mkoa wa Tabora mara tu baada ya kuzinduliwa, naomba mkisome kwa makini ili mzielewe fursa na vivutio vya uwekezaji vilivyopo Tabora, kisha mzitumie  kuzalisha mali kwa manufaa yenu, Mkoa na Nchi kwa ujumla.

 

Mwisho, napenda kuwapongeza wanahabari wote wa Mkoa wa Tabora kwa ushiriki wenu katika Kikao hiki kifupi.

Ahsanteni kwa kunisikiliza

…………………………

Dkt Philemon Sengati

MKUU WA MKOA WA TABORA

04.05.2021

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa