Leo Tarehe Septemba 15, 2023 Ndugu Abdallah Shaibu Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji uliopo kata ya Ntalikwa wenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni mia sita zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji unaosimimiwa na TUWASA ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji.
Akiongea na wananchi, Ndugu Abdallah Shaibu Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru 2023, amesema baada ya kupitia nyaraka zote ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huu kwakuwa umefuata taratibu zote muhimu ikiwepo kufanya tathmini ya athari za kimazingira katika eneo la mradi na nyaraka zote za mradi zikiwa zimeandalia kikamilifu.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi sita (6) ambayo leo Septemba 15, 2023 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023 Manispaa ya Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa