• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MWAKYEMBE AKEMEA UHARIBIFU WA MAENEO YA KIHISTORIA KWA LENGO LA KUTAFUTA MADINI

Posted on: March 15th, 2019

MWAKYEMBE AKEMEA UHARIBIFU WA MAENEO YA KIHISTORIA KWA LENGO LA KUTAFUTA MADINI

SERIKALI imewataka wananchi kuacha tabia ya kuharibu maeneo ya kihistoria ikiwemo majengo ya kale kwa madai potofu kuwa kwenye maeneo hayo wakoloni walificha madini ndani yake.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.

Alisema vitendo vya aina hiyo vinasababisha Serikali kutumia gharama kubwa pindi wanapotaka kukarabati na kurudisha historia ya maeneo hayo.

“Hakuna ambaye ni mjinga aweke ndani ya nyumba dhahabu halafu asiifuate…hata wangekuwa wameweka mali ndani ya majengo yao wamekuja na njia nyingine ya kutaka kuendeleza maeneo hayo kwa kuweka miradi ya kuchimba visima ili wachukue madini kama yangekuwepo” alisema.

Mwakyembe alisema maeneo hayo ni muhimu sana katika Historia ya Tanzania na pia katika ukuzaji wa utalii kwa ajili ya kulipatia Taifa fedha za kigeni.

Aliongeza kuwa maeneo hayo ni muhimu katika kutoa elimu kwa vijana wa kitaifa kufahamu historia ya nchi yao kwa ajili ya kuwa wazalendo wazuri wa Tanzania.

Mwakyembe alisema Wizara yake inaewndelea na utaratibu wa kuyaorodhesha maeneo yote ya kihistoria kwa ajili ya kuyahifadhi na kuyakarabati kwa ajili faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha Waziri huyo alisema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ambayo utafanya maeneo ya kihistoria yasiguswe na kuzuia uharibifu.

Alisema baada ya muswada huo kupitishwa na hatimaye kuwa Sheria utasaidia kulinda utajiri wa urithi wa Kihistoria ulipo hapa nchini usiweze kuharibiwa na kupotea.

Katika hatua nyingine Mwakyembe alisema Serikali itahakikisha inarudisha nchini Fuvu la Kichwa cha Mama Shujaa mpiga ukoloni wa Kijerumani kutoka Singida Bibi Liti.

Alisema Shujaa huyo aliweze kupambana na Wajerumani kwa kutumia nyuki hadi hapo aliposalitiwa na wenzake na hatimaye Wajerumani wakata kichwa chake na kuondoka nacho.

Mwakyembe alisema lazima fuvu la kichwa lirudishwe nchini na kuhifadhiwa katika jumba maalumu kwa ajili ya historia ya Tanzania

 

Mwisho 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MHE. CHACHA AIPONGEZA TIMU YA UMISSETA MKOA KWA KUSHIKA NAFASI YA TATU KITAIFA

    July 01, 2025
  • RC. CHA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA, WAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UADILIFU.

    July 01, 2025
  • TABORA: MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA MAADILI YA NCHI

    June 26, 2025
  • MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA YAENDESHA MAFUNZO MAALUM YA MATUMIZI YA MFUMO WA PEPMIS KWA WATUMISHI WA UMMA MKOA WA TABORA

    June 23, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa