Wakazi wa Kijiji cha Kaliua Mshariki Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora, ni rasmi sasa wameondokana na adha ya kusaka maji umbali mrefu zaidi ya Kilometa 10 baada ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2023 kuzindua mradi Mkubwa wa Maji kijijini hapo, septemba 16, 2023.
Mradi huo umezinduliwa leo, na Kiongozi wa Mbio hizo Mwenge Mwaka huu, Abdalla Kaim, ambapo amepongeza wasimamizi wa mradi huo kwa kusimamia vyema mradi hadi kukamilika kwake.
Mradi huo ambao umetekelezwa na TUWASA umegharimu kiasi Cha Sh. Milioni 503 fedha kutoka Serikali Kuu.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mhe. Aloyce Kwezi Mara baada ya Mwenge kuzindua mradi huo, amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo mkubwa na wenye tija kwa wananchi wa Kaliua hadi kukamilika na kueleza kuwa sasa wananchi wa Kijiji hicho na Kaliua kwa ujumla watapata maji safi na salama.
Mradi huu wa Ujenzi wa Shule ya Msingi Dkt. Samia ni miongoni mwa miradi sita (6) ambayo imepitiwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Ambapo Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Dkt. Chuachua aliupokea kutoka Wilaya ya Tabora
Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Tabora Septemba 14, 2023 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge. ambapo utahitimisha mbio zake ukiwa umezindua jumla ya miradi 50 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2 na kukabidhiwa Mkoa wa Singida Septemba, 21, 2023.
Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa