Katika kuhakikisha utunzaji wa mazingira unatekelezwa kikamilifu, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Ndugu Abdalla Shaib leo Septemba 17, 2023 umezindua mradi wa Shamba la Miti ekari 19 lenye miti 12,886, Wilayani Urambo. Mradi huu umegharimu shilingi Milioni 37.7 kwa ajili ya shuguli za upandaji sambamba na uendeshaji.
Akisoma taarifa ya Mradi huu, Ndugu Amon Philipo Joel ameeleza kuwa “Mradi huu una uwezo wa kunufaisha wakulima wapatao 400 wenye uwezo wa kulima ekari 2.5 kila mmoja. Sambamba na utunzaji Bioanuwai na Ekolojia ya eneo la shamba na maeneo yanayozunguka shamba. Kufyonza hewa ya ukaa ambayo dio chanzo kikuuu cha athari ya mabadiliko ya tabia nchi, kutumika kama shamba darasa kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali, pia ni chanzo cha nishati na ajira kwa wakulima wa tumbaku.”
Mradi huu wa Shamba la Miti ni miongoni mwa miradi nane (8) ambayo itapitiwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo. Ambapo Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Kenani Kihongosi aliupokea kutoka Wilaya ya Kaliua
Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Tabora Septemba 14, 2023 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge. ambapo utahitimisha mbio zake ukiwa umezindua jumla ya miradi 50 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2 na kukabidhiwa Mkoa wa Singida Septemba, 22, 2023.
Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa