Mkimbiza Mwenge Kitaifa 2023 Ndugu,Adallah Shaib Kaim leo Septemba 16, 2023 amezindua mradi wa Ujenzi wa Shule ya Msingi Dkt. Samia iliyopo Kijiji cha Mwendakulima, Wilayani Kaliua, ujenzi huu umegharimu kiasi cha shilingi milioni 578, ambapo kiasi cha shilingi milioni 561.1 zilitoka kwa Wahisani na Shilingi Milioni 17 mchango ya wananchi na jumla ya wanafunzi 900 kufaidika na mradi huu.
Akisoma taarifa ya mradi, Afisa Elimu Wilaya Shadraki Kabanga amesema “awali wanafunzi walikuwa wakitembea umbali wa kilomita 10 kwenda kupata elimu vijiji vya jirani, hali iliyosababisha watoto wengi kucha kwenda shule. Na hivyo uwepo wa shule hii kutasaidia kutoa nafasi kwa watoto kupata elimu kwa urahisi. Na mwisho alimshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi kwenye sekta ya elimu.
Mradi huu wa Ujenzi wa Shule ya Msingi Dkt. Samia ni miongoni mwa miradi sita (6) ambayo itapitiwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Ambapo Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Dkt. Chuachua aliupokea kutoka Wilaya ya Tabora
Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Tabora Septemba 14, 2023 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge. ambapo utahitimisha mbio zake ukiwa umezindua jumla ya miradi 50 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2 na kukabidhiwa Mkoa wa Singida Septemba, 21, 2023.
Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa