Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Septemba 17, 2023 umepokelewa Wilayani Urambo, ukitokea Wilaya ya Kaliua na kuanza kukimbizwa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa ajili ya kukagua,kuona, kuzindua pamoja na kuweka Mawe ya Msingi katika miradi nane (8),ya Maendeleo ikiwemo ya Elimu, Afya, Maji na Barabara yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Kenani Kihongosi ameupokea Mwenge huo Septemba 17, 2023 na kukimbizwa umbali wa kilomita 47 na kuzindua miradi nane (8) yenye thamani ya Bilioni 2.6
Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Tabora Septemba 14, 2023 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge, na kuhitimisha mbio zake na kukabidhiwa Mkoa wa Singida Septemba, 22, 2023, ukiwa umezindua jumla ya miradi 50 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2, katika Halmashauri zote nane (8).
Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa