Ndugu, Abdallah Shaibu, Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2023 amekagua, kutembelea na kisha kuzindua mradi wa Upandaji Miti uliopo Shule ya Msingi Manoleo. Mradi huu unajumuhisha miti 1000, ambapo miti 900 ni ya kivuli na miti 100 ni ya Matunda iliyotolewa na TFS Tabora.
Mradi huo wa miti ina lengo la kuunga mkono juhudi za kuhifadhi vyanzo vya maji na mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Mradi huu una thamani ya shilingi Milioni 1.7
Aidha, mradi huo unawapatia uzoefu na mafunzo wanafunzi wa Shule ya Msingi Manoleo kupitia shughuli ya Umwagiliaji na uwekaji wa chupa chilizi.
Baada ya kuzindua mradi huo, Ndugu, Abdallah Shaibu, Kiongozi wa Mbio za Mwenge alipanda mti kama mfano wa kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa mazingira.
Mradi huu wa vijana ni miongoni mwa miradi sita (6) ambayo imepitiwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Tabora. Ambapo Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Peter Bura aliupokea kutoka Wilaya ya Sikonge.
Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa