NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja ameutaka uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori(Tawa) kusimamia zoezi la wavamizi wa Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima iliyopo wilayani Kaliua wanaondoa mazao yao ambayo yamekomaa.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tawa inaendesha shughuli zake za uhifadhi wa mazingira na wanyapori bila kikwazo chochote.
Naibu Waziri huyo alitoa kauli hiyo jana katika kijiji cha Wachawaseme kilichopo eneo la Isawima wilayani kaliua mkoani Tabora alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara .
Alisema kwamba uhifadhi ni muhimu na wenye manufaa makubwa ya taifa na wananchi kwa sasa na vizazi kijacho na hivyo Serikali haiwezi kuacha watu wavamiea na kuharibu maeneo hayo.
Mary alisema kwamba kutokana uamuzi huo wa wakulima walivamia eneo hilo wanatakiwa kuondoa mazao yao kwa utaraibu maalumu utakaopangwa na Serikali kupitia vibali ambavyo vitabainisha nini mkulima alichonacho kwenye hifadhi hiyo ili kuweza kutambua nani ni nani anaingia kenye hifadhi muda husika .
Alisema serikali haiwezi kuona watu wanavamia hifadhi zilizohifadhi kisheria na kuharibu miundombinu yake kwa sababu ya maslahi ya watu wachache na kuharibu manufaa ya watu wengi nchini.
Aidha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ameingiza serikali ya mkoa na Tawa kuhakikisha kuwa watakapokamilisha zoezi la kuondoa mazao yao kwenye hifadhi hakuna mtu yoyote anayeingia ndani ya hifadhi kwa ajili ya shughuli zozote ya kibinadamu zinakinzana na uhifadhi.
Alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia hifadhi hiyo kuendelezwa kwa mshoroba wa wanayama na maji kuendelea kutirika hadi ziwa Tanganyika kwa asilimi 30.
Hata hivyo aliahidi kutuma wataalum wa kupima mipaka kwa ajili ya kuelimisha wananchi wa vijiji 11 vilivyomo kwenye eneo la Isawima ili kutambua mikapa yote ya kila kijiji na mwisho wa eneo ambalo wananchi hawapaswi kuingia wala kufanya shughuli za kibinadamu.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Kamati ya Ardhi na maliasilia na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la kaliua Aloyce Kwezi alimweleza Naibu waziri huyo kwamba wananchi wa eneo la Isawima ambalo eneo lake kubwa ni Hifadhi wanaomba kutambua mikapa yake eneo lao .
Alisema kwamba kutokutambua mipika hiyo kumesababisha baadhi wa wananchi kuingia eneo la hifadhi na kufanya shughuli za kibinadamu.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati alisema uongozi wa Mkoa hauwezi kuona watu wachache wanatumia fedha zo na kuingia katika eneo hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibindamu.
Alisema eneo hilo ni muhimu kuhifadhiwa kwa kuwa ni chujio la maji yanayoelekea Ziwa Tanganyika na ni mazalia ya Nzige wekundu.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa