Leo Julai 6,2023 Ofisi ya Mrajisi Msaidizi pamoja na Ofisi ya Kilimo Mkoa wa Tabora zimesimamia jumla ya Wenyeviti 300 wa AMCOS Mkoani Tabora katika zoezi la utolewaji wa Elimu ya Bima Mazao iliyotolewa na kusimamiwa na Shirika la Bima la Taifa NIC. Utolewaji wa elimu ya Bima imeanza kwa wenyeviti wa AMCOS za wakulima wa Tumbaku.
Hatua hii ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian aliyoyatoa Februari 14, 2023 alipofanya ziara ya ukaguzi wa mashamba ya Tumbaku yalioathiriwa na mvua ya mawe wilayani Sikonge.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa