Katika kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye maboresho ya sekta ya elimu, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian leo Julai 18, 2023 amepokea madawati na viti mia mbili na hamsini (250) vyenye thamani ya Shilingi Milioni 25 kutoka Banki ya NMB kanda ya magharibi.
Akipokea madawati hayo, ameipongeza na kuishukuru Bank ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono Serikali katika sekta ya elimu ambapo shule mbili(2) za Msingi na zingine mbili (2) za Sekondari kufaidika na msaada huo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa