Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na ofisi ya MkufunziMkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoa wa Tabora imeendesha kikao kazikwa wataalam wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi. Kikao hichokimefanyika leo katika ukumbi mdogo wa Isike Mwanakiyungi,lengo ikiwa nikujadili changamoto zinazowakabili watu wazima wasiojua kusoma na kuandikapamoja na mikakati ya kuboresha programu nyingine za elimu kwa kundi hilimuhimu.
Mafunzo haya ni sehemu ya juhudi za kuboresha elimu mkoa wa Tabora, hasakatika kuimarisha utoaji wa elimu kwa watu wazima. Lengo kuu ni kupangamikakati ya utekelezaji wa majukumu ya elimu ya watu wazima kwa mwaka 2025, ilikuhakikisha kuwa mkoa unafikia malengo yake ya kuondoa ujinga na kutoa fursasawa za elimu kwa wote.
Kikao hiki kinahusisha maafisa elimu kutoka wilaya zote za mkoa wa Tabora nakinatarajiwa kudumu kwa siku mbili. Mafunzo haya yanatarajiwa kuwa na manufaamakubwa katika kuboresha elimu ya watu wazima na kuimarisha elimu nje ya mfumorasmi mkoani Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa