• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

PAMBA YOTE KUNUNULIWA –WAZIRI MKUU

Posted on: July 18th, 2019



PAMBA YOTE KUNUNULIWA –WAZIRI MKUU

 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipatia ufumbuzi tatizo la kusuasua kwa masoko ya pamba nchini baada ya kufanya mazungumzo na wadau muhimu wa zao hilo na kufikia muafaka.

 Lengo ni kutaka  kuhakikisha pamba yote inanunuliwa ifikapo mwaka mwishoni mwa Mwezi huu na wakulima wanalipwa pesa zao zote.

 Ameyasema hayo leo (Jumatatu 15, 2019) wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika Kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga .

 Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imeshafanya mazungumzo na Benki Kuu na Benki mbalimbali ili ziweze kuzikopesha  Kampuni mbalimbali za ununuzi wa pamba ili zihakikishe zinanunua pamba yote ya wakulima nchini.

 Alisema wamefanya mazungumzo na wanunuzi wa pamba,Wakuu wa Mikoa inayolima pamba,viongozi wa mabenki na Gavana wa Benki kuu na kufikia makubaliano.

 Waziri Mkuu alisema wanunuzi walishindwa kununua pamba yote kwa pesa zao kwa vile hawakuweza kukopeshwa na benki ambayo nayo hayakuhakikishiwa dhamana na Benki kuu.

 Alisema baada ya mazungumzo wamekubaliana Benki kuu ya Tanzania kuanza kutoa dhamana kwa benki ambayo nazo zitatakiwa kutoa mikopo kwa wanunuzi wa pamba.

 Alibainisha makubaliano hayo sasa yanafungua mlango wa wanunuzi kununua pamba yote ya wakulima tena kwa pesa taslimu na sio mkopo.

 Aidha Waziri Mkuu,aliwaonya wanunuzi kutotumia pesa wanayopata kufanya mambo tofauti na badala yake waitumie kununulia pamba pekee.

 Waziri Mkuu aliwapongeza wakulima kwa kuzalisha  na kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka tani 135,000 mwaka 2017,mwaka 2018 tani 220,000 na mwaka huu wanatarajia kupatikana tani zaidi ya 300,000.

 Kwa upande wa Waziri wa Kilimo,Japhet Hasunga alisema uzalishaji wa pamba msimu huu unaweza kuongezeka hadi kufikia tani kati ya 300,000 hadi 350,000.

 Aidha alisema maghala mengi ya pamba  hayana ubora na kwamba wanafanya jitihada kuhakikisha yanakuwa na ubora sio kama ilivyo sasa.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri,alisema wamefanikiwa kuwafanya wakulima walime kwa tija kwa kuongeza uzalishaji kwa kilo kutoka kilo 300 hadi 800 kwa ekari.

 Awali Mkuu wa Wilaya ya Igunga,John Mwaipopo,alisema wakulima walikuwa bado hawajapeleka pamba zikiwa bado majumbani huku wale waliopeleka ghalani,kuwa bado hawajalipwa.

 Mbunge wa jimbo la Manonga,Seif Gulamali alisema kuwa wakulima wana hali mbaya kutokana na kutouza pamba yao na hivyo kushindwa kufanya mambo ya msingi kama kujikimu kwa chakula na gharama zingine za maisha.

 Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewashauri wakulima wa mazao mbalimbali hapa nchini kujenga utaratibu wa kuweka mipango mizuri ya kujiandaa ya kilimo kijacho kwa kuweka akiba kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo.

 Alisema Serikali haiwezi kutoa pembejeo kwa kila zao la Mkulima hapa nchini badala yake ni jukumu la wakulima kujenga utaratibu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya uboresahaji wa kilimo kijacho

Mwisho.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa